Waigizaji wakike weusi wamekuwa ni chachu ya kuendelea kwa tasnia ya filamu nchini marekani(Hollywood) na wamekuwa wakifanya vizuri kila kukicha mfano wa waigizaji hao ni Halle Berry , Janet Jackson and Thandie Newton.
Ufuatao ni mtiririko unaoonyesha gharama za waigizaji hao wanavyo lipwa;
1: Halle Berry : Malipo : ($80 Million) :
Mrembo huyu wa Hollywood anayevutia hata kimuonekano ndiye anayeshikilia nafasi ya kwanza kimalipo ya juu sana kama dollar Million 80 kwa filamu,Halle Berry ameshiriki kwenye filamu kama 007 James Bond ,Catewomen , Monsters Ball na nyinginezo nyingi.
2: Rosario Dawson : Malipo : ($50 Million) :
Rosario Dawson mwanadada huyu muigizaji alipata umaarufu sana baada ya filamu ya king of the jungle ambayo ilifanya vizuri sana katika ulimwengu wa filamu lakini filamu kama Alexander , Rundown , Death Proof and Unstoppable zilizidi kuthibitisha kuwa alihitajikan kwa dau kubwa sana kutokana na uwezo aliouonyesha.
3: Thandie Newton : Malipo : ($44 Million) \
Thandie Newton Umaarufu ulikuwa mkubwa zaidi baada ya filamu ya “Mission: Impossible II” na kufanikiwa kuingia mikataba ya projekti kubwa ya filamu 2004 alifanya filamu iliyofanikiwa kufanya vizuri inaenda kwa jina la CRASH akafanya filamu kama The Pursuit of Happyness ambayo iliwekaa kumbukumbu kama moja kati ya filamu bora.
4: Zoe Saldana : Malipo: ($38 Million) :
Mwanadada huyu alianza fahamika rasmi toka kwenye filamu ya Center stage lakini alipata umaarufu zaidi katika filamu kama Crossroads, Pirates of the Caribbean: The Curse of the Black Pearl and Vantage Point,pia mwanadada huyu alikuwepo ni mmoja kati katuni zilizotumika katika filamu ya avatar,Colombiana ni filamu aliyoicheza kama mhusika mkuu na ilimletea umaarufu na mafanikio makubwa.
5: Gabrielle Union : Malipo : ($33 Million) :
Mwaka 1999 alifanikiwa kutokea katika filamu ya “She’s All That” na uwezo wake mkubwa aliouonyesha ulipelekea kupatamikataba mikubwa lakini umaarufu ulikuwa zaidi alipoachia filamu ya “Bring It On” na mwaka 2003 ulikuwa mwaka mzuri kwake baada ya kuachia filamu tatu kwa mkupuo Cradle to the Grave , Bad Boys 2 , and Deliver Us from Eva.
6: Kerry Washington : Malipo : ($31 Million) :
Mwanadada huyu alifahamika zaidi katika ulimwengu huu wa filamu mwaka 2000 pale alipo shiriki katika filamu ya “Our Song”,lakini pia “Bad Company” ni filamu aliyoicheza kama mhusika mkuu ambayo ilionyesha uwezo wake kwa kiasi kikubwa na kumpa nafasi kubwa katika tasnia ya filamu hollywood,na mwaka 2003 alishiriki katika filamu ya “Peeples” ambayo ilizidi kumpandisha juu zaidi.
7: Paula Patton : Malipo : ($25 Million) :
Mwanadada huyu alianza pata shavu baada ya filamu ya “Hitch” ila kibarua kilizidi pamba moto baada ya filamu ya "Precious" ambayo yeye alicheza kama “Ms Blu Rain” ,Pia alishiriki katika mfululizo wa series ya Mission Impossible Ghost Protocol ambayo iliweka record katika ulimwengu wa filamu hollywood.
8: Meagan Good : Malipo : ($20 Million) :
Friday ni filamu ambayo uwezo wake ulionekana katika filamu hiyo ambayo mrembo huyu alicheza kama mhusika mkuu kwa jina la Tina. na mwadada huyu ameolewa na DeVon Franklin ,Mwaka 2012 haukuwa mbaya kwake alifanya filamu kama Anchorman 2: The Legend Continues , Don Jon.
9: Lesley-Ann Brandt : Malipo : ($18 Million) :
Mwanadada huyu ni moja kati waigizaji bora katika tasnia hii ya filamu hollywood na amepata mafanikio makubwa kupitia filamu kama \Spartacus , Drift , and A Beautiful Soul.
10: Gugu Mbatha-Raw : Malipo : ($13 Million) :
Mrembo huyu ambaye kibarua kilianza kupamba moto rasmi baada ya filamu ya “Holby City” aliyoshiriki kama Collette Hill,na baada ya hapo alifanikiwa kufanya filamu kama “Bad Girls , Belle Fantastic Four , Beyond the Lights .