Sunday, November 9, 2014

JE UNAHITAJI KUFANIKIWA NA KUISHI MAISHA UYATAKAYO? HII NDO NJIA SAHII.......


HAKI YA KUFANIKIWA
Ni mengi yanasemwa kuhusu kufanikiwa na kuwa tajiri,mfano wengine husema mafanikio hufuata mkondo,Wengine husema mafanikio ni mipango ya mungu na huja kwa yule aliyechaguliwa au kutunukiwa,haya ni machache na mengine mengi husemwa  nisengependa tuongelee sana kuhusu hayo kwani si lengo letu,Lengo letu ni kutaka kujua kwanza nani ana haki ya kufanikiwa?
Maswali yanakuja kama ifuatavyo:
1.Unadhani una haki ya kufanikiwa?
2.Kwanini hufanikiwi?
3.Lini utafanikiwa na kwa kiwango gani?


                           1.UNADHANI UNA HAKI YA KUFANIKIWA
Watu wengi ukiwauliza swali hili hakuna hata mmoja atakayejibu sina haki ya kufanikiwa,lakini majibu yao  hayaendani na vitendo vyao,mawazo yao na mwenendo wao wa maisha kwa ujumla ndo maana hawafanikiwi.
Uthibitisho ni kama ifuatavyo:
1.Je ulishawahi kufikilia hata siku moja kwamba siku moja utakuwa milionea katika maisha yako?
2.Je ni hatua zipi ulichukua baada ya kufikilia hivyo?
Nisengependa nikujibie hilo swali ila niseme kwamba bila kuwa na fikra basi hakuna kitu chochote kinaweza fanyika/tendeka/tokea lakini fikra tu pekee hazitoshi lazima huwe na hatua madhubuti utakazo zichukua ili kufanikisha picha iliyondani ya fikra zako.
                              2.KWANINI HUFANIKIWI
Watu wanapenda sana kufanikiwa na kuwa matajiri kama bilgate,Henry ford n.k lakini ni watu wachache kati ya hao wengi wanaojiuliza:
1. kwanini sifanikiwi?,
Ukijiuliza kwanini sifanikiwi basi ndo itakuwa hatua ya kwanza kutafuta njia sahihi za kuweza kufanikiwa,Jiulize ni mara ngapi umejiuliza swali hilo?,
2.Je ni uamuzi gani ulichukuwa baada ya kujiuliza?
Mazunguzo ya mwanasayansi Albert Einstein na Daktari
Einstein:Tofauti kati ya mimi na nyinyi ni kwamba mimi huwa natumia akili ya Mungu.
Daktari;Akili ya mungu?
Einstein;Ndio.
Daktari;Kivipi?
Einstein;Huwa najiuliza maswali magumu ambayo sinauwezo wa kuyajibu na kisha nayatafutia majibu nikipata majibu yake huwa nadhani Mungu ndo amenipa majibu.
kwakufanya hivyo huwa natumia akili ya mungu.

Je ni nini tunajifunza kutoka kwa mazungumzo hayo?
Ni rahisi tu,ni kwamba njia pekee ya kutatua matatizo ni kujiuliza maswali,Amini au usiamini swali la kwanini sifanikiwi ni moja kati ya maswali magumu sana katika ulimwengu wa maswali na laiti kama lingekuwa jepesi basi leo kusengekuwa na tabaka la watu masikini ulimwenguni,baada ya kujiuliza na kujijibu kinacho fuata ni utekelezaji wa majibu yako kwani swali hili haliishi tu kwenye kujibu bali na utekelezaji.
                                    3.LINI UTAFANIKIWA NA KWA KIWANGO GANI
Hili ni swali muhimu sana katika ulimwengu huu wa mafanikio na ni watu wachache sana hujiuliza,
Sababu za umuhimu wake;
-Bila kujua lini huwezi jua mwendo unaokwenda nao ni sahihi au sio?
-Bila kujua kiwango sahihi cha mafanikio yako ni ngumu kujua umefanikiwa na kufikia malengo au bado.
-Bila kujua kiwango na muda hauta fahamu kwa usahihi ni shughuli ghani ufanye,unaweza ukajikuta unafanya shughuli yoyote hile,Mfano mtu mwenye malengo ya kuwa milionea baada ya miezi sita akauze karanga za kukaanga msingi shilingi elfu kumi,kwa hiyo kwa uwezo wa kawaida tu unajua hapa malengo hayawezitimia,
Kwa hivyo panga muda ambao ni sahihi na kiwango cha mafanikio inakuwa vizuri zaidi kama unapanga kiasi cha pesa ambacho unahitaji kuwa nacho kwa wakati huo,
                                                 HITIMISHO
Kila mtu anastahili kufanikiwa awe mlemavu,mzima,mwenye uwezo mkubwa wa kufikiria,mwenye uwezo wa kawaida na wengineo,kikubwa ni kufuata mambo muhimu yanayostahili kufuata ili kufikia mafanikio.
INAENDELEA................................