KUNA MAZINGATIO YA KUFIKIA MAFANIKIO
Baada ya kuona nani anastahili kufanikiwa na kwanini anastahili kufanikiwa tunaingia katika sehemu ya pili ya ya "njia sahihi za kufanikiwa na kuishi kwa mafanikio" nayo ni;
MAZINGATIO YA KUFIKIA MAFANIKIO.
Kabla hatujaanza ningependa nikukumbushe kitu kimoja,ili mtu aweze kuishi maisha ya uhuru,amani,furaha na upendo basi lazima mtu huyo afanikiwe na kuwa tajiri,Najua unaweza pingana na kauli hii ila ngoja nikueleze kitu kila mwanadamu anaishi kwa kutimiza matakwa ya vitu vitatu navyo ni;.
1.Mwili(Body)
2.Nafsi(Soul)
1.Mwili
Mtu hawezi kuishi maisha yaliyokuwa ya furaha na ukamilifu kama asipo timiza mahitaji ya mwili wake yaani kama vile chakula kizuri,Mavazi mazuri,Malazi bora mfano nyumba kubwa nzuri na hivi vyote vinahitaji pesa.
2.Nafsi(Soul)
Ili maisha yawe ya ukamilifu na furaha pia mwanadamu anahitaji kuitimizia nafsi yake mahitaji kama Mapenzi na mapenzi umekuwa wimbo wa kinyonge sana kwa masikini,kwani furaha ya kubwa ya mwanadamu inapatikana kutoka kwa yule ampendae lakini mtu asiyekuwa na uwezo hawezi hata kujaza nafasi yake kama baba bora wa familia yake kwani mahitaji mengi yanahitaji uwepo wa pesa.
3.Akili(Mind)
Mtu hawezi kuishi kikamilifu,amani na furaha kama hajatimiza mahitaji ya Akili/ubongo wake nayo ni kupata vitabu na muda wa kuvisoma,kuzungukwa na vitu vya thamani vitakavyo mfanya ajisikie raha,kutembelea sehemu mbali mbali na kutarii,
Mahitaji hayo matatu ni mambo tunayoyafanya kila siku ya maisha yetu huenda kwa kukusudia au laa lakini hayo ni mambo muhimu ambayo kila mtu anayahitaji.bila pesa mambo hayo ni ngumu kutimia tena sio pesa kidogo nyingi zinahitajika hadi kufikia hapo hatunabudi kukubaliana mtu hawezi kuishi kikamilifu na kwa furaha na upendo bila ya kufanikiwa na kuwa tajiri,hakuna mtu anayeridhika na kidogo lakini pia kutaka kikubwa sio dhambi,hivyo kuna haja ya watu kufundishwa mazingatio ya kuzingatia ili kufanikiwa na kuwa matajiri.
Najua umesikia njia nyingi na mambo mengi kuhusu namna ya kufanikiwa na kuwa tajiri mfano;
-kupunguza matumizi
-kuhifadhi sana
-wengine hata wizi ikiwezekana
-kuomba sana punguzo la bei
Onyo:
Hakuna hata njia moja iliyo ya kweli hapo juu kuhusu kufanikiwa na kuwa tajiri huenda hufahamu tajiri ni nani? ngoja nitakueleza lakini kwanza nikueleze udhaifu wa kwanini usitumie hizo njia hapo juu.
--kupunguza matumizi
huenda sifahamu kuhusu matumizi ila nachokijua hakuna matumizi mabaya ,madhumuni makuu ya kutafuta nikutumia sasa kwanini unapunguza matumizi,kupunguza matumizi ni kulazimisha kile kidogo kikutosheleze
yaani ni sawa na yule bwana anayetaka kuridhika na kidogo,tumia tu kisipotosha ndo ujue kwamba kipato chako ni kidogo na unahitaji kukiongeza kuna msemo unasema "ubongo ni kama umeme ukiutumia vizuri utapata mambo mazuri kama mwanga,nguvu kuendesha vifaa kama pasi,tv,radio lakini ukiutumia vibaya unaua" ni nini maaana yake? jibu kama tutafanya kipato kidogo kitutosheleze basi kamwe hatutaweza tafuta njia za kuweza kupata kikubwa zaidi hivyo hatutaweza kuwa matajiri bali watu wa kipato cha kati yaani hawana tofauti kubwa na masikini.
--kuhifadhi sana
Kwanini unahifadhi sana na unataka kufanikiwa na kuwa tajiri ?
Mtu anayehifadhi sana huyo ni tajiri tayari,Akiba imetokana na ziada,Maana ya ziada ni kwamba baada ya kukidhi mahitaji yote sasa kile kilicho baki ndo akiba,je ni kweli unahifadhi baada ya kukidhi mahitaji yako yote jibu si kweli bali ni kupunguza baadhi ya matumizi,tunarudi pale pale kupunguza matumizi hivyo sina haja ya kueleza saaana hii sio njia sahihi,sababu kwanza inadumaza ubongo ambao ndio silaha kubwa ya kufanikiwa na kuwa tajiri pia inatulazimisha turidhike na kidogo kitu ambacho sio sahihi.
-kuomba sana punguzo la bei
Kuomba saaana punguzo la bei sio njia nzuri ya kuelekea mafanikio na kuwa tajiri,bali unachotakiwa kufanya ni kupima thamani ya bei na umuhimu wa kile kitu kwako,kama thamani ya kitu ipo juu kuliko bei basi nunua kwa bei yoyote ila kama kinyume chake achana nacho.
-wengine hata wizi ikiwezekana
Kuiba sio njia sahihi ya kufanikiwa na kuwa tajiri japo kuwa wapo watu wachache wamefanya hivyo,huenda ni kwasababu hatumjui tajiri ni nani lakini ngoja nikukumbushe kuwa heshima na kunyenyekewa ni moja kati ya sifa za tajiri,jamii haiwezi kukuheshimu na kukunyenyekea kama wewe ni mwizi,Ebu tazama mtu kama Henry Ford vile ambavyo jamii inamuheshimu,Pia wizi unadumaza uwezo wa ubongo kwenye kufikiria kutokana na upatikanaji wa pesa yako pia utaiba mara ngapi?
Hivyo hii sio njia sahihi ya kufanikiwa na kuwa tajiri. Najua unahitaji kuja ipi ni njia sahihi hata kama ningekuwa wewe ningefanya hivyo hivyo subiri sitakupa njia ya kufikia tu malengo na mafanikio yako bali ni utatuzi wa yale yanayokusibu,Nilikuwa kama wewe sikujua la kufanya nilihitaji njia isiyokuwa na ugumu na iliyoweza nifikisha katika malengo yangu hivyo sasa nimekuwa muelezeaji ya njia hizo hata wewe utakuwa hivyo hivyo si tu kufanikiwa bali shuhuda wa njia bora za kufanikiwa na kuishi kwa mafanikio..................itaendelea