Tuesday, November 18, 2014

NJIA YA KWANZA KULEKEA MAFANIKIO(SEHEMU YA SITA)

Leo ningependa  tujiulize nini tunahitaji na kwanini? bila shaka jibu lake ni jepesi tu, mafanikio na kuwa matajiri itakuwa ni ajabu tusipo mjua huyu tajiri na mtu aliyefanikiwa ni nani?
Jibu:
Mtu yeyote mwenye uwezo wa  kumiliki vyote vile avitakavyo kwa ajili ya kuishi au maisha yake hayatakayo,basi mtu huyo amefanikiwa na kuwa tajiri.Mtu ambaye si tajiri hawezi kuishi maisha yale hayatakayo kwani hadi maisha ya kawaida sana kwa sasa yanahitaji kiasi kikubwa cha pesa kuna haja kubwa ya watu kufundishwa elimu  hii kwani ndo njia sahihi ya kutimiza malengo liyonayo.
Kuna vitu ambavyo huenda hukuwahi jiuliza ila leo ningependa ujiulize,



-Hivi nani alidhani ungefika wakati tungeweza pata mayai bila uwepo wa kuku?
-Hivi nani alidhani kwamba ungefika wakati tungepata bidhaa kama milango siling board bila uwepo wa mbao?
Huenda kuna kitu bado hujatambua ila ukweli ni kwamba kama utahitaji kufanikiwa basi utafanikiwa na kujiuliza haya mafanikio yalikuwa wapi siku zote hizo,kikubwa kufuata mazingatio.
Linaweza likawa ni wazo geni kwako ila amini katika swala la mafanikio hakuna aliyejuu kuliko wenzake hata hapo ulipo kama huna kitu lakini kama utafuata mazingatio basi utapanda toka hapo ulipo hadi kufikia mahali ambapo wewe utakuwa wa kwanza kujiuliza ilikuaje ulifika hapo,
.HATUA YA KWANZA KUELEKEA MAFANIKIO
1.FIKRA/KUFIKIRI
"Kuna kitu au sehemu  ambayo ndo chanzo cha uzalishaji wa kila kitu ulimwenguni hapo ndipo picha ya vitu vyote uandaliwa kabla havija  tolewa rasmi katika hali ya kuonekana".
FIKRA;
Ndio kitu pekee kinachoweza kuzalisha mawazo mengi ambayo yanaweza kukupelekea kufanikiwa na kuwa tajiri,huenda ikawa njia ya ambayo hujawahi sikia na ukahisi si ya ukweli lakini ngoja nikwambie hii ndo njia pekee ambayo haitakugharimu hata shilingi na pia utayafikia malengo yako kwa ukubwa zaidi,Je unamfahamu Henry ford,bilgates,Thomas A.Edison na wengine wengi hawa ni baadhi tu ya watu waliofanikiwa bila hata msingi zaidi ya fikra/kufikiri kwao kama ulikuwa hufahamu ukiamini uwezo wa fikra/kufikiri kwako basi utajua nini ufanye na haitakupelekea tu kuwa na mafanikio na kuwa tajiri bali kuwa na uwezo wa kutatua matatizo na kuwa mtu ambaye kila mtu atatamani kuwa kama wewe.
Tambua hili kabla hujafanya au kuamua lolote "Ubongo ni kama umeme kama utatumika vizuri basi utaleta matokeo mazuri ila kama utatumika vibaya basi unaweza hata ukasababisha kupoteza maisha" Ni watu wangapi wana weka picha za uchi au wanauana bila sababu za msingi? na je ni watu wangapi wanafanya uvumbuzi wa teknolojia mpya au vitu vipya?,kati ya hao watu wa aina mbili unaweza dhani huyo wa kwanza kama hana ubongo na hafikirii lakini ukweli ni kwamba ukiutumia vibaya basi ubongo sio kitu kizuri kabisa,
-Kwanini leo tut\naongelea ubongo na wakati sisi tunataka mafanikio?
Hakuna mtu aliyefanikiwa asiyejua ni vipi atumie ubongo au fikra alizonazo kuzalisha na azilishe kwa kiasi gani,njia zipi atumie na akina nani ashirikiane nao,
-Je fikra/kufikiri kwa mtu aliyefanikiwa au anayetaka kufanikiwa zikoje?
Laiti kama mafanikio yangekuwa rahisi basi kila mtu angefanikiwa kwanza lazima utambue hilo hivyo usochoke kufikiria namna gani utafanikiwa,fikiri ni wapi unaweza fanya kitu ,nini unaweza fanya kulingana na hapo ulipo na kwa kiasi gani kitakulipa.
Muda wote huwe ni mtu wa kutaka kupata kikubwa kwani mafanikio hayaletwi na kitu kidogo.Usipoteze muda kufikiri au kufanya vitu visivyo na mchango fanikiwa kwanza,kwani kama ni marafiki utawapata wengi na wazuri pale utapokuwa na mafanikio,Hakikisha unatumia muda mwingi kufikiri nini ufanye na hakikisha hupotezi wakati bila kufanya hivyo kwa siku.
-Yesu alisema"Kama mtayaamini yale mnayo yafikiria pindi mnasali mtayapata na yatakuja mikononi mwenu"
Kwanini alisema kama mtayaamini yale mnayo yafikiria,sababu alijua kufikiri ndo njia pekee inayoweza leta majibu sahihi katika yale maswali hujiulizayo,Henry Ford yeyen alifikiria kutengeneza kitu chenye miguu minne kitakacho tembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine leo ni mmoja wa matajiri wakubwa marekani na ulimwenguni kote kupitia magari ya Ford,
Hii njia itakayokupa mafanikio na Utajiri bila hata shilingi lakini kikubwa fikiri kwa upana kulingana na hali9 halisi ya wewe ulivyo kama utakuwa wa kwanza kuamini huwezi kufanikiwa basi amini huwezi na hata usijaribu kwani hauta fanikiwa ila kama unaamini basi fanya na utafanikiwa tumia muda mwingi kufikiri na fikra zitakupa jibu sahihi.