Sunday, November 16, 2014

NJIA SAHIHI ZA KUFANIKIWA?(SEHEMU YA TANO)

Baada ya kuona mambo mengi ambayo wengi tulidhani ni njia sahihi za kufanikiwa lakini kumbe ndani yake zilikuwa na changamoto nyingi leo tujikite na zingatio ili ambalo ni zingatio la mwisho kabla hatuja anza njia zetu za kuelekezana kwenda katika milango itakayo badilisha maisha yetu na kufanya tuishi ndoto zetu.
Kama ulikuwsa hufahamu ngoja nikueleze kama ilivyokuwa algebra na formula zake kwenye hesabu basi kufanikiwa nako ni sayansi inayotumia fomula zake pia na bila kuzingatia fomula hizo uwezi fanikiwa uthibitisho:
-Watu wangapi wanafanya biashara ya aina moja mwingine anafanikiwa na mwingine hafanikiwi?
-Watu wangapi wenye elimu ya kiwango sawa mwingine anafanikiwa mwingine hafanikiwi?



Yapo mambo mengi yakuthibitisha ila ukweli ni kwamba bila kuzingatia njia sahihi za kufanikiwa basi mafanikio kwako yatakuwa wimbo ambao utausikia kwa wengine huenda umesahau ngoja nikukumbushe ,hakuna kitu rahisi kama kunywa maji au kula chakula lakini kama usipo tumia njia sahihi au mpangilio basi tegemea kukabwa au kupaliwa na chakula hicho au maji.
Kufanikiwa hakuhitaji mazingira kwani kama mafanikio yangekuwa ni mazingira basi leo tusingeona tabaka la masikini na matajiri kwenye kila kona ya dunia na miji mikubwa,kama tunaona watu wanaishi katika mazingira ya aina moja na wanafanya kazi zinazo shabihiana na mmoja anafanikiwa na mwingine hafanikiwi hii inamaanisha kufanikiwa kunahitaji formula inayohitaji kufatwa huenda watu wakawa wanafuata formula hizi bila kujua au kwa kujua na kujikuta wanafanikiwa,Japo kufanikiwa hakuhitaji mazingira simaanishi mtu aende katikati ya jangwa la sahara na ategemee kufanya biashara itakayomfanya afanikiwe hapana.kwani mafanikio yanahitaji kushirikiana na watu na hapa ndipo msaada wa mazingira unaweza wafanya kazi.
Pia kufanya vitu kwa ufasaha hakuhitaji uwe na kipaji bali ni kuzingatia tu kwani ni wangapi wenye vipaji vikubwa sana hawafanikiwi na na wangapi wenye vipaji vya kawaida wanafanikiwa?,
Pia kufanikiwa na kuwa tajiri hakumaanishi kwamba unafanya vitu ambavyo wengine wameshindwa kufanya kwani watu wanaofanya biashara ya aina moja wanafanya karibuni kila kitu kinachofanana lakini mmoja anafanikiwa na mwingine hafanikiwi.
Kulingana na haya yote hatunabudi kufikia hitimisho kwamba kufanikiwa na kuwa tajiri kunahitaji kufanya mambo katika njia sahihi au kufuata hizo fomula.na kila mtu atakaye fuata fomula hizo basi l;azima afanikiwe.
Je hizo fomula ni ngumu sana kiasa kwamba wachache wanafanikiwa na wengine hawafanikiwi?
Jibu:Hapana njia hizo sio ngumu kama unawezo wa kusoma na kuzingatia tu,kama tulivyoona na  tunavyoendelea kushuhudia katika jamii watu wenye akili wanafanikiwa na wale tunaowaona hawana akili wanafanikiwa pia,wenye maumbo makubwa wanafanikiwa na wenye maumbo madogo wanafanikiwa pia ,hivyo basi hii inaonyesha kuwa yeyote anaweza fanikiwa kikubwa kufuata mambo vile yanavyo stahili kufuatwa au fomula.Amini utafanikiwa na utashangaa wapi mafanikio haya yametoka hakunaga kujaa kwa nafasi wala kuchelewa katika ulimwengu waa mafanikio.kikubwa soma na zingatia maneno haya,
Je kama kuna watu watu wanafanikiwa ndani ya nchi yako kwanini wewe usifanikiwe?Je kama kuna watu wanafanikiwa ndani ya mji ambao wewe unaishi kwanini na wewe usifanikiwe?
Pia sikwamba ni sababu ya kufanya biashara fulani au uwe na elimu fulani kwani watu wanafanikiwa kupitia hiyo hiyo ambayo unayodhani sio na majirani zao wenye kama hiyo wanabaki masikini,
 HAYO NI MACHACHE TU UNAYOSTAHILI KUZINGATIA KUFIKIA KILELE CHA MAFANIKIO AMINI,ZINGATIA NA LAZIMA UTAFANIKIWA.