Baada ya kupata muda mwingi wa kutafakari kuhusu elimu na mafanikio ebu tuendelee ili tuweze kujua elimu inamchango gani katika kufanikiwa au haina.
Kabla sijaendelea na hilo ngoja nikwambie kitu kama ifuatavyo;
1.Ili mtu afanikiwe sio lazima awe na hii wanayoiita wao elimu.
2.Kuwa na elimu sio kitu kibaya
3.Elimu na mafanikio ni mafanikio ni vitu viwili tofauti.
Tahadhari:Mafanikio inatumika kama lugha ya mjumuisho.
Baada ya kufika mahakamani na kesi kuanza wakili wa gazeti la "chicago newspaper" alisema yeye atathibitisha kwamba Henry Ford(Muasisi wa magari maarufu ya ford) hajaelimika kupitia ushahidi wa huyohuyo Mr.Ford,kama hujui Mr.Ford elimu yake ni chini ya gredi/darasa la sita.
Basi kesi ikawa kama ifuatavyo
Wakili:Benedict Arnold ni nani Mr.Ford?
Mr.Ford:Simjui
Wakili:Ni askari wangapi uingereza ilituma marekani kupambana na waasi mwaka 1776?(Maswali haya yalikuwa ni ya madarasa ya chini sana)
Mr.Ford:Sijui.
Mr.Ford:Akaongezea japo sifahamu ni kias gani idadi ilikuwa ila nachojua walikuwa wametumwa wengi kuliko idadi ambayo ilitumwa kabla hapo nyuma .
Wakikili akataka kuuliza swali lingine Mr.Ford akamkatisha kwa kumnyooshea kidole na kumwambia "Laiti kama ningetaka kujibu maswali yako ya kipumbavu kwenye meza yangu ni mpangili wa vibonyezo ambavyo nikibonyeza anaweza akaja kijana ambaye nimemuajili kazi yake kujibu maswali tu ya biashara yangu ambayo mimi nimewekeza akili na jitihada zangu basi huyo angejibu na haya maswali yako,akaendelea kusema ebu nambie sababu ya mimi kuacha kazi zangu na kuanza kujifunza taaluma itayoniwezesha kujibu maswali tu?Wakati nina vijana walionizunguka wakisambaza taaluma ninayohiitaji(yaani uhandisi wa magari ya ford)?" basi maswali yale yalimlowesha kabisa wakili na kila mmoja ndani ya mahakama aligundua kwamba majibu yale hayakuwa majibu ya mtu mjinga bali ni majibu ya mtu mwenye ELIMU.
Najua hadi kufikia hapa ujui ni nini uamue ngoja tujiulize tena,
1.ELIMU NI NINI?
2.MTU ALIYE ELIMIKA NI NANI?
Basi amini usiamini ila kila mtu ameelimika kama atajua wapi atapata taaluma pale akihiitaji,pia aweze vipi kutumia taaluma hiyo katika malengo fulani,kwa msaada wa uwezo wake wa kufikiri.
Mifano;
Japo Henry Ford aliishia darasa la sita lakini alijua ni taaluma gani anahiitaji na wapi ataipata kwa kufanya hivyo leo ni moja kati ya matajiri wakubwa marekani.
Pia japo Thomas A.Edison alikaa darasani kwa miezi mitatu tu katika maisha yake yote lakini alijua wapi apate taaluma na ni vipi aitumie na kwa sasa ni moja kati ya matajiri .
Hivyo sihitaji kuendelea sana kukwambia kwamba hata bila ya kwenda darasani mafanikio yapo pale pale kikubwa ni wewe kujua unastahili kufanikiwa hivyo kupigana kupanda mbegu za mafanikio.Watu wengi hawafanikiwi sababu wao wenyewe huamini haiwezekani kwao kufanikiwa zingatia vitu vifuatavyo;
1.Mafanikio hayaji kwa watu wa kawaida hivyo usikubali kuwa wa kawaida amini unastahili kila kubwa ulionalo ndani ya hii dunia.
2.Amini unaweza kuwa tajiri na kuishi maisha ya mafanikio makubwa kuliko mtu yoyote ulimwenguni.usiamini kwamba kamwe huwezi kuwa juu kuliko fulani katika ulimwengu wa mafanikio kikubwa ni kufikiri na kuweka njia za kufanikiwa zaidi.
3.Usipendelee kukaa na wale wanaojiita wao masikini tumia muda mwingi kusoma au kufikiria namna gani utafanikiwa na ukishafanikiwa wapelekee mkate wao wa kila siku(msaada) kama chakula kwao huoni watu waliofanikiwa wanavyotoa misaada.
4.Usishindane na mtu yoyote shindana na ndoto zilizo ndani ya kichwa chako hivyo utakuwa wa ajabu ukipanga mambo madogo yatokee kwenye maisha yako.
5.Usikate tamaa pale unapoanguka bali iwe changamoto ya kujifunza kuhusu kesho ili kubwa lisije tokea
6.Panga mipango mingi sana kwakufanya hivyo utakuwa mtumiaji mzuri wa muda na ukifanikiwa basi utaingiza kikubwa sana.
7.Hakuna tofauti ya mtu anayekula na anayejiandaa kula hivyo kama unajiandaa kufanikiwa kuanzia sasa ishi kama mtu aliyefanikiwa,na siku zote jihisi kama umeshafanikiwa
8.Kikubwa zaidi jifunze kugeuza hasara kuwa faida,Mfano umepoteza simu ya laki nane basi amini imepotea ili ikupe changamoto ya kununua mpya,na usifikirie kwanini imepotea.
9.Usiangalie wala kusikiliza chombo cha habari kinacho zungumzia kuhusu masuala ya umasikini kwani umasikini wewe huna faida nao katika maisha yako hata ukijua nchi gani masikini,umasikini unamadhara gani yote hii aina maana bali jifunze kujua namna gani utakuwa na mafanikio makubwa zaidi ,wapi naweza fanikiwa na ni nini nahitaji,kwa kukafanya hivyo hautajirudisha nyuma .Pia amini hata kama watu wote watakuwa masikini amini wewe si watu wote hivyo lazima utafanikiwa tu.
10.Kila siku imba nyimbo kuhusu mafanikio ikiwezekana kila uamkapo jiambie lazima nitafanikiwa na kuishi maisha ya mafanikio,kama hujui mafanikio huja kwa kusikia ,kuona,kusoma hivyo kufanya hivyo utajipa njia nyingi zitakazo kuletea mafanikio.......................................................
Yapo mengi sana bado unastahili sikia kuhusu kufanikiwa na kuwa tajiri lakini kikubwa zingatia ila ahadi yangu kwako ni kwamba hautafanikiwa tu bali utakuwa shahidi kwa wale wanaolia kuhusu umasikini.TUKUTANE SEHEMU YA TANO KUPEANA NJIA SAHIHI HII NI UTAMBULISHO TU NA KUKUWEKA TAYARI KUPOKEA NJIA HIZO.