Saturday, November 22, 2014

NI VIPI FIKRA AU KUFIKIRI KUNAVYOWEZA KUKULETEA MAFANIKIO(NJIA YA KWANZA KUELEKEA MAFANIKIO)

(HAKUNA MTU ASIYE NA FIKRA SAHIHI KUHUSU MAFANIKIO AMBAYE AMEFANIKIWA,HUENDA ALIFANYA KWA KUKUSUDIA AU KUTOKUKUSUDIA KUFIKIRI KUTAKA KUFANIKIWA)
Tunaendelea na njia yetu ya kwanza ambayo ni fikra/kufikiri kuelekea kwenye mafanikio,Ebu tujiulize;
1.Kama hufikirii namna gani utafanikiwa je mafanikio yatakuja kwa njia gani kwako?
2.Je kama wewe huna muda wa kufikiria kuhusu mafanikio ndani ya maisha yako unadhani nani atafanya hivyo kwa ajili yako?



Watu wengi hupoteza muda mwingi kwenye vitu kama;
-Vipindi vya Televisheni
-Vipindi vya radio
-Kuchat kupitia simu,kompyuta n.k
Lakini je tujiulize unadhani kutumia muda katika mazingira haya ni ni njia sahihi ya sisi kufikia yale tunayoyaita mafanikio?
Bila shaka kupitia njia hii hatuwezi pata fikra zitakazo tujenga na kutufanya tufanikiwe na kufikia yale tunayoita mafanikio,sisemi usitazame vipindi vya televisheni lakini nasema kwanini usitafute njia itakayo leta LG inch 40 Flat,Dstv na glasi kuubwa ya maziwa  huku ukitazama vizuri hivyo vipindi upendavyo hivyo kwa sasa tumia muda mwingi kutafuta hiyo njia badala ya kutumia muda mwingi kwenye televisheni yako ya nchi kumi na saba ,sisemi usichat na marafiki facebook,twitter n.k ila nasema kwanini usitumie muda mwingi kufikiria njia itakayo kuletea vifaa bora na kuboresha maisha yako ili uchat vizuri na hao marafiki,Hivi utajisikiaje ukichat huku pembeni una glasi kubwa ya juisi, mkononi una Iphone 6 bila shaka huko ndo kuchat kuzuri,nachosema ni kwamba vijana wengi hawajipi nafasi ya kufikiri na kutafuta njia bora za kuwawezesha kufikia malengo yao.Pia hawazipi fursa uwezo wao wa kufikiri kukaa na kupata muda wa kutafakari kama tuliweza kupata mayai bila kuku na tukapata bidhaa kama milango bila uwepo wa mbao hivi unadhani kupitia uwezo huo hauwezi kukuletea mawazo makubwa ya kukufikisha unapopataka basi amini utafanikiwa na hata utajiuliza yalikuwa wapi mafanikio hayo.
Nilihitaji kukueleza na utambue kwamba mafanikio si lazima huwe na ile wanayoiita elimu ili nawewe ufahamu kwamba unahaki ya kufanikiwa kwani elimu ni elimu na mafanikio ni mafanikio,Itakuwa ni swala la ajabu kama usipofanikiwa na ikiwa unahaki ya kufanikiwa hivi huoni wanao endesha magari ya milioni mia mbili,manyumba makubwa ambayo hata hukuwahi fikiri siku moja utakuwa ni mmoja kati ya watakao miliki,Amini utafanikiwa sababu huna sababu ya kutofanikiwa na kufanikiwa ni rahisi zaidi kuliko hata kutofanikiwa,Kama unatumia muda mwingi kufikiri ni nini ufanye,wapi ufanye na kwa wakati gani,basi amini ukipata majibu ya maswali  yako itakuwa ni njia itakayo kupeleka kule ambako mafanikio yaliko huna haja ya kufikiria mambo madogo sababu kama mtu unayetaka fanikiwa utakuwa wa ajabu kufanya hivyo amini mambo makubwa yapo kwa ajili yako na una haki ya kuyamiliki,Kwanini ujilinganishe na wale sababu wana hali ya chini basi ngoja nikiupe siri amabayo unastahili kuwa nayo wakati wote,Usilinganishe uwezo wa kufikiri wala mali ulizonazo na mtu mwingine yeyote kwani katika ulimwengu wa mafanikio hakuna kushindana bali kupamabana kuhakikisha unakuwa juu na ndoto zako zinatimia.Mafanikio hayatakuja bali kwa wale wanaofuata njia au mkondo wa kufanya mambo kuelekea katika mafanikio,Fikiria mambo makubwa ambayo ukifanya yataleta mafanikio kwako na kutimiza malengo yako.
Mfano ;Kwanini ushindane na bakharesa kwa kuuza mikate wakati unaweza kuwa mkulima mkubwa wa ngano na kumuuzia bakharesa ili atengeneze hiyo mikate,Hivyo si njia nzuri kushindana sababu mara nyingi huwa mahitaji yake ni kupata mshindi na si kuleta mafanikio na ugunduzi .
Siku zote lazima utambue kwamba"Ubongo ni kama umeme ukiutmia vizuri basi utakupa nguvu au nishati itayoweza kukupa mwanga,kuendesha mitambo na kufanyan vingi vizuri ambavyo  unavyovihitaji lakini kama ulivyo umeme unaua kama ukitumiwa vibaya basi na ubongo ndivyo hivyo hivyo ulivyo" Jiulize ni wangapi wanatembea bila nguo?,wangapi wanavuta madawa na kusababisha vifo vyao? hivi unadhani hawana ubongo wa kufikiri jibu hapana,Basi ukweli ni kwamba kama utautumia ubongo kukupa njia za kuweza kuhakikisha unafanikiwa utafanikiwa na hata kujiuliza yalikuwa wapi haya mafanikio lakini kama utautumia vibaya na kujikakatisha tamaa basi utakuwa wa kwanza kujiletea umasikini na hata utajuta kwanini uliletwa kwenye dunia hii tunayoishi.Kama ilivyo mtu anavyoweza fikiria ni namna gani anaweza fanikiwa na kuwa tajiri huenda kwa kukusudia au kwa kuto kukusudia ndivyo hivyo hivyo mtu anaweza kuwa masikini na kupanda mbegu zitakazo leta umasikini mkubwa kwake kwa kukusudia au kutokukusudia,haijalishi awe na ile wanayoiita elimu au asiwe nayo.
UNAHAKI YA KUFANIKIWA NA KWANINI UFANIKIWI? FIKIRI KATIKA NJIA SAHIHI KWANI UTAFANIKIWA NA HATA KUJIULIZA YALIKUWA WAPI HAYAFANIKIO.