Baada ya kuona mambo ambayo watu wengi hudhani ndo njia sahihi za kufanya ili kufikia kilele cha mafanikio (Sehemu ya 1 na 2) lakini kumbe sikweli bali ndio sababu zinazo wafanya wazidi kurudi nyuma hata wengine kukata tamaa kwamba siku moja watafanikiwa na kuishi maisha ya mafanikio,Hizi ni changamoto tu nazokupa ambazo wewe ulidhani ni njia sahihi kumbe sio laiti kama ningekuwa wewe ningekuwa na shauku kubwa yakutaka kujua funguo hizo zitakazo nifungulia milango ya mafanikio,Zamani nilikuwa kama wewe pale nilipokuwa nikitafuta njia zitakazo niongoza kufikia kilele cha mafanikio,siku moja nikasikiliza kipindi cha radio walikuwa wakisema punguza kununua vitu kama vocha,pombe,soda na vitu vingine ambavyo kwao walisema havikuwa na umuhimu sana,huwezi amini sikuwahi fanikiwa hata siku moja kutimiza yale yaliyokuwa yakisemwa kwasababu ndio vitu nilivyokuwa vinapamba maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana mfano mara nyingi nilihitaji kununua vocha niongee na mpenzi wangu hivyo sikuweza acha kununua wakati mwingine kuongea tu na marafiki wa mda mrefu,pia sikuweza kuacha kununua vitu kama soda sababu nilipokuwa sina lakufanya na kuhisi mpweke nilipendelea tumia vinywaji laini kama hivyo kwa hiyo ikafika wakati nikaamini kwamba daaah kuwa na mafanikio na kuishi maisha ya mafanikio ni kitu kigumu sana.
Lakini kumbe sikweli unajua hata pua na mdomo ni majirani wa karibu saaana lakini pua akiamua kwenda mtembelea mdomo na akapitia njia ya toka chini ya miguu itamchukua miaka kumkaribia mdomo lakini akifanya kama yanavyofanya mafua basi n i dakika tu anafika kwa mdomo,kikubwa sikuwa na njia sahihi za kufika nilipotaka kufika hivyo ulifika wakati nilikata hadi tamaa,Amini nikuambiacho ipo njia ya kuwa na mafanikio makubwa kuliko hata uwezo wa akili na umri ulionao,Ukizingatia nikuelezacho basi utafanikiwa na kujiuliza haya mafanikio yalikuwa wapi siku zote hizi,Huenda hujui ili ngoja nikwambie;
-Una haki ya kufanikiwa
-Ni rahisi kufanikiwa kuliko kutofanikiwa
-Ila kila kitu kina namna ya kutokea,maana:(mafanikio na kutofanikiwa vyote vina mbegu itategemea umepanda mbegu gani?)
Kama kweli unasoma na kuzingatia sasa utakuwa ni mtu ambaye kwa kiasi kikubwa sana umebadilika kimtazamo sababu naamini sehemu ya kwanza na ya pili ilikuwa na mchango mkubwa sana kwako,ukihisi huna mabadiliko rudia tena kusoma sehemu ya kwanza na ya pili kabla hatuja fika sehemu ya nne,
Sasa utakuwa unaamini kwamba;
- una haki ya kufanikiwa
-Mafanikio yapo kwa ajili yako
-Mafanikio yanapatikana kwa kupanda mbegu za mafanikio
-Na umepenga lini unataka huwe umeshafanikiwa
TAHADHARI:
Kama unahisi unasoma ilikupoteza muda basi ni moja kati ya watu wanaofanya makosa makubwa sana sababu haya ninayokueleza hutokuja sikia sehemu yoyote zaidi ya hapa,hivyo kuwa makini hii ni njia sahihi
ya wewe kubadilka na kuishi maisha ambayo ulikuwa ukiyaota tu.
Leo tujadili kuhusu ELIMU,JE UNAFIKIRI ELIMU NDIO SABABU YA MTU KUFANIKIWA NA KUISHI MAISHA YA MAFANIKIO?
Najua hadi kufika hapa unajiuliza nafikiria nini hadi nauliza swali ambalo wewe unahisi jibu lake ni la wazi kwamba "NDIO" .
Basi ngoja nikueleze usichokijua laiti kama ningekuwa wewe nisinge jibu swali hili bila kuuliza, elimu ni nini?
Ngoja nizidi kukueleza kile usichokijua hivi Unafahamu kwamba, kila mtu asili yake anayo elimu?
Ngoja nisikujibu sasa hadi pale utakapoelewa nisemacho,Vijana wengi kutoka vyuoni ndio wamekuwa wa kwanza kuidharau elimu waipatayo na moja kati ya maswali yao ni haya hivi kweli nitafanikiwa kupitia hiki nikipatacho? Asilimia sitini huamini haiwezekani hizo chache tu zinazo amabatana naye,Ukweli ni kwamba elimu tu pekee haitoshi kukufanya ufanikiwe na kuishi maisha ya mafanikio uthibitisho;
-Ni watu wangapi wamefanikiwa bila kupita huko elimu inako tolewa
-Watu wangapi wameajiliwa na hao tunaowaita wasio na elimu
-Ni maprofesa wangapi wenye mvi wanafanya kazi ya ualimu vyuoni na kulipwa mshara duni wa milion mbili hadi tatu?
Huenda ufahamu mafanikio ni nini ?,huenda hujawahi kuona watu waliofanikiwa,huenda hujui ni watu wanao ingiza kiasi gani kwa siku?.
Unahisi mshahara wako wa milioni moja kwa mwezi ni mafanikio ninayo ongelea hapa?
Kama unafikiri hivyo basi umefanya kosa kubwa sana,Kwa mwaka unaingiza umejitahidi milioni ishirini hayo ni mafanikio? acha masihara,Nyumba ya milioni thelasini unaijenga zaidi ya miaka miwili hayo unaita ni mafanikio?
Mafanikio nayoyazungumzia hapa sio hayo.
Tuendelee na elimu baadaye utafahamu,utaamini na utafanikiwa sababu mafanikio yapo kwa ajili yetu.
Hakunaga kujaa kwa nafasi katika ulimwengu huu ninaoongelea,wala haita tokea siku utajaa nafasi,
Elimu pekee haitoshi kumfanya mtu afanikiwe bali kama elimu itaelekezwa kule ambapo mafanikio yanapatikana basi huenda ikawa moja kati ya vitu ambavyo vitamsaidia mtu aweze kufanikiwa,Wasomi wengi na maprofesa wamekosa taaluma hii ya kuifanya ielekee kwenye mafanikio na iwalipe pesa nyingi kutokana na kushindwa kufanya hivyo leo tumekuwa na maprofesa wengi watumwa ndani ya vyuo vikuu ambao wanalipwa pesa ndogo sana kulinganisha na muda waliopoteza kusoma na kupata hiyoi wanayoiita elimu,
Natumai hadi kufika hapa umepata mwanga ni nini nacho ongelea sasa ngoja nikujibu maswali yako kuhusu elimu naamini hadi nikiweka nukta ya mwisho utaamini kwamba elimu pekee haitoshi.
Kwanza tujiulize ,
1.ELIMU NI NINI?
2.MTU ALIYE ELIMIKA NI NANI?
Educate imetokana na neno la kilatini "Educo" maana yake ni "Eduse"
Eduse maana yake ni kuvumbua/kutengeneza/toa fikra/ kutoka ndani ya (Ubongo)
MTU ALIYE EL IMIKA NI NANI?
Kipindi cha vita ya dunia gazeti la "CHICAGO NEWS PAPER" moja kati ya machapisho yalisema kwamba
Henry Ford ( Muasisi wa magari maarufun ulimwenguni ya Ford) kwamba hana elimu na silolote bali ni mjinga tu kama wajinga wengine hivyo Mr.Ford alichukia na kupeleka kesi hiyo mahakamani....................
KAMA HENRY FORD MGUNDUZI WA MAGARI YA FORD NI MJINGA MTU MWENYE ELIMU YUKOJE? NISENGEPENDA KUKUELEZA SASA NINI KILIENDELEA MAHAKAMANI KAA FIKIRI TUKUTANE SEHEMU YA NNE UJUE NINI KILIENDELEA NA ELIMU ITAKUSAIDIAJE KAMA UTAITUMIA.......................................................